KARIBU

KARIBU
Tunakusalimu katika Jina la BWANA wetu YESU KRISTO. karibu katika ukurasa huu maalumu wa USCF CCT UDOM CHAPLAINCY-KITIVO CHA TIBA. USCF ni kifupisho cha maneno machache; UNIVERSITY STUDENTS CHRISTIAN FELLOWSHIP na CCT ni kifupisho cha CHRISTIAN COUNCIL OF TANZANIA. Sisi ni ushirika wa vijana wa vyuo vikuu kutoka makanisa wanachama wa baraza la kikristo Tanzania (CCT). tumekuwa na ukurasa huu maalumu kwa ajili ya Kuhubiri Injili, Kufundisha Neno la Mungu, kupashana habari pamoja na kushauriana. Ni kiu yetu kuwa walioko makazini, majumbani, mashuleni na maeneo mbalimbali waweze kufikiwa na mahubiri/mafundisho yetu yanayotolewa na watumishi mbalimbali waliopo katikati yetu na wale wa nje ya USCF pamoja na wahubiri wa kimataifa. KARIBU TUJIFUNZE NA KUHABARIKA NA MUNGUAKUBARIKI

Leo jumapili mtumishi Samweli mwaimu katika kanisa la tiba akifundisha neno linalosema

MSAADA WA MUNGU MAISHANI MWETU
Kutoka 14:21-31, katika maisha yetu tunaona msaada wa Mungu kwenye maisha yetu haupo.Msaada wa Mungu upo kwenye maisha yetu endapo tutampenda.
Mara nyingi tunaaza na jitihada zetu na kumuacha Mungu lakini Mungu anataka tuanze na yeye, katika maisha yetu Duniani tumepewa nafasi ya miungu tunachofanya kinatokea na kwetu tunavyowasaidia wengine tunamhudumia Mungu na Mungu anavyokuwa jirani na wewe anakujibu maombi yako. Fedha ushauri, mawazo.
Vile unavyotaka kutendewa ndivyo uwatendee wengine(kipimo mnacho wapimia wengine ndichomtakachopimiwa)

No comments:

Post a Comment

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Yohana 3;16