KARIBU

KARIBU
Tunakusalimu katika Jina la BWANA wetu YESU KRISTO. karibu katika ukurasa huu maalumu wa USCF CCT UDOM CHAPLAINCY-KITIVO CHA TIBA. USCF ni kifupisho cha maneno machache; UNIVERSITY STUDENTS CHRISTIAN FELLOWSHIP na CCT ni kifupisho cha CHRISTIAN COUNCIL OF TANZANIA. Sisi ni ushirika wa vijana wa vyuo vikuu kutoka makanisa wanachama wa baraza la kikristo Tanzania (CCT). tumekuwa na ukurasa huu maalumu kwa ajili ya Kuhubiri Injili, Kufundisha Neno la Mungu, kupashana habari pamoja na kushauriana. Ni kiu yetu kuwa walioko makazini, majumbani, mashuleni na maeneo mbalimbali waweze kufikiwa na mahubiri/mafundisho yetu yanayotolewa na watumishi mbalimbali waliopo katikati yetu na wale wa nje ya USCF pamoja na wahubiri wa kimataifa. KARIBU TUJIFUNZE NA KUHABARIKA NA MUNGUAKUBARIKI

ABOUT US

USCF ni ushirika wa wanafunzi wa Kikristo wanaotoka katika makanisa wanachama wa jumuiya ya 
kikristo Tanzania (CCT). Katika hatua za sekondari ushirika huu ulikuwa ukifahamika kama UKWATA. Katika chuo kikuu cha Dodoma (Udom), USCF iko katika ulezi wa CCT chini ya mchungaji wetu mpendwa Baba Timothy Erasto Chimeledya. Aidha kanisa letu la hapa Udom limekuwa katika vitivo vitano yaani, Elimu, Tiba, Informatics, Social sciences na Humanities. USCF CHAS ni moja kati ya hivyo vitivo ambapo kimefahamika zaidi kama kitivo cha tiba. Katika kitivo chetu cha tiba Uscf ilianzishwa mnamo mwaka 2011 chini ya mwenyekiti Ayoub Mtulo. Tangu wakati huo ushirika wetu umeendelea kuwalea wanachama kimwili na kiroho pamoja na kuhudumia jamii inayotuzunguka. Tumeendelea kutoa huduma kupitia watumishi wetu wanaokwenda kuhubiri katika makanisa na mikutano pamoja na uimbaji. Katika uimbaji tumekuwa na kwaya pamoja na vikundi binafsi ambavyo Mungu ameendelea kuwahudumia watu wake kupitia vipawa hivyo. Tunapenda kuwakaribisha watu wote ambao wanapenda kushirikiana nasi pasipo kujali tofauti za madhehebu ili tuweze kumtukuza Mungu pamoja. Msingi wa imani yetu ni wokovu aliotyuletea Mungu kupitia kwa mwanawe mpendwa Yesu Kristo, tunamwamini Mungu Baba Mwwnyezi, Tunamwamini mwanwawe wa pekee Yesu Kristo na Roho Mtakatifu aliye nafsi yangu Mungu. Amen.

No comments:

Post a Comment

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Yohana 3;16