KARIBU

KARIBU
Tunakusalimu katika Jina la BWANA wetu YESU KRISTO. karibu katika ukurasa huu maalumu wa USCF CCT UDOM CHAPLAINCY-KITIVO CHA TIBA. USCF ni kifupisho cha maneno machache; UNIVERSITY STUDENTS CHRISTIAN FELLOWSHIP na CCT ni kifupisho cha CHRISTIAN COUNCIL OF TANZANIA. Sisi ni ushirika wa vijana wa vyuo vikuu kutoka makanisa wanachama wa baraza la kikristo Tanzania (CCT). tumekuwa na ukurasa huu maalumu kwa ajili ya Kuhubiri Injili, Kufundisha Neno la Mungu, kupashana habari pamoja na kushauriana. Ni kiu yetu kuwa walioko makazini, majumbani, mashuleni na maeneo mbalimbali waweze kufikiwa na mahubiri/mafundisho yetu yanayotolewa na watumishi mbalimbali waliopo katikati yetu na wale wa nje ya USCF pamoja na wahubiri wa kimataifa. KARIBU TUJIFUNZE NA KUHABARIKA NA MUNGUAKUBARIKI

MALENGO YA KANISA 2016/2017



UNIVERSITY STUDENTS’ CHRISTIAN FELLOWSHIP 
USCF-CCT UDOM CHAPLAINCY-TIBA



MALENGO YA KANISA LA USCF-TIBA KWA MWAKA WA HUDUMA 2016/2017
Mithali 16:
 1 ‘maandalio ya moyo ni ya mwanadamu
bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA’’
3‘ mkabidhi BWANA kazi zako na mawazo yako yatathibitika.’
9‘moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.




UTANGULIZI
      Ndugu wanaUSCF ninawasalimu katika jina la Bwana wetu Yesu kristo….
      Tunamshukuru Mungu kwa kibali na neema ya kuwepo kwa ushirika huu (USCF) unaotuunganisha kupitia Yesu Kristo mwokozi wetu
      Kipekee tunawashukuru wana USCF wote wa kanisa la TIBA,  kwa namna ambavyo tumeendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali na kwa moyo wa kujitoa ambao tumeuonesha katika utumishi huu.
Aidha, tunapenda kuweka wazi kuwa katika awamu mpya hii ya uongozi, lazima tuwe na dira ambayo itatuongoza kupitia MALENGO ambayo kanisa tunatamani kuyafikia katika kipindi hiki cha mwaka mmoja.
Malengo haya ni mjumuisho wa malengo katika kamati mbalimbali za kanisa , mjumuisho huu ni maafikiano ya kikao cha baraza kuu la kitivo cha tar. 05.06.2015.
Ifahamike kuwa kamati tulizonazo katika kanisa ni ;
       kamati ya Uinjilisti
       kamati ya maombi
      Uimbaji (kikundi cha kusifu na kuabudu na kwaya)
       Fedha,mipango na Usafirishaji
       kamati ya Mapambo
      Kamati ya vyombo
      Kamati ya akina mama na akina dada
      Kamati ya taaluma na maktaba


MALENGO
Lengo la kwanza
     Kubuni na kuanzisha chanzo cha mapato (income generating source) ili kupata jibu la kudumu la changamoto ya kifedha katika kitivo chetu.
    Katika kufanikisha hili kamati kuu ya kitivo itaunda kamati ya kuratibu lengo hili na punde tutaitangaza mbele ya kanisa na hivyo ilete jibu ni mradi gani tunaweza tukaanzisha na namna ya kufanikisha.
Lengo la pili
 kufanya ununuzi wa vyombo vya muziki vifuatavyo;
     i.        Kinanda aina ya MOTIF
   ii.        Booster
  iii.        Mike za ngoma (drums)
  iv.        Nyaya za mike nne na mike za waya mbili na
   v.        Tranka kubwa la utunzaji wa baadhi ya vifaa vya muziki.

Lengo la tatu;
    Kufanikisha semina tatu za kutoka nje kama zitakavyoratibiwa na kamati ya uinjilisti, maombi na uimbaji. Pia kuwa na semina za ndani kwa kadri nafasi na ratiba ya kanisa itakavyoruhusu.
 Lengo la nne;
    Kufanya ziara za nje mbili zitakazohusisha kamati za uinjilisti, maombi na uimbaji ( kwaya na kikundi cha kusifu na kuabudu), kwa kuungana katika huduma katika ziara husika.

Lengo la tano
  kufanya mikesha mitatu kila muhula wa masomo ( semister), yaani wa kufungua muhula, kufunga muhula na mmoja wa kati ya muhula
 Lengo la sita         
 kufanikisha yafuatayo katika kamati ya uimbaji ;
     i.        Kufanikisha kurekodi mkanda wa picha (Video shooting) wa pili wa kwaya yetu MAGUGU NA NGANO
ii.  Kurekodi mkanda wa sauti wa tatu wa kwaya yetu
iii. Kurekodi mkanda wa kwanza wa sauti (audio) wa kikundi cha kusifu na kuabudu (praise and worship team) na kadri itakavyowezekana kurekodi mkanda mmoja wa picha (video).
iv. Kusaidia kufanikisha malengo ya vikundi mbalimbali vya uimbaji tulivyonavyo kanisani.

lengo la saba
Kufanikisha yafuatayo katika mambo ya kijamii;
i.Kufanya bonanza mbili kila muhula wa masomo (semister)
ii. Kununua vifaa vya michezo vitakavyotumika tunapokuwa na bonanza
iii. Kufanya hafla ya kuwaaga wanafunzi wenzetu wa udaktari mwaka wa tatu (MD3) wanapoondoka kwenda kwenye mafunzo ya vitendo.
iv.Kutembelea wenye uhitaji.
v. Kujumuika na wenzetu katika matukio ya  arusi na misiba na
vi.Kuimarisha familia zetu ndani ya USCF


Lengo la nane
Kuwa na maombi ya mfungo maalum kama kanisa kila mwisho wa mwezi  na maombi ya mfungo katika  vikundi vya uimbaji kadri utakavyowekwa na kuridhiwa na vikundi husika
Lengo la tisa
Kuwa na semina maalum ya mafundisho  kwa ajili ya wadada na wamama itakayoratibiwa na kamati ya wanawake.
Lengo la kumi
   Kufanya matengenezo ya FRAME ya mapambo, kununua mto maalum wa madhabahuni utakaotumika katika kupiga magoti panapohitajika.
   Pia kununua vyombo imara vya chuma (stand mbili kwa ajili ya vyombo vya sadaka).
Lengo la kumi na moja
 Tuwe na flash disk yenye ukubwa wa 16GB kwa ajili ya kuhifadhi nakala za mitihani mbalimbali iliyopita, vitabu vya taaluma zetu na pia vya kiroho (SOFT COPIES) kwa ajili ya kusaidiana kitaaluma na kiroho pia .
  Pia kununua mafaili ya kuhifadhia katika namna ya hard copies.






HITIMISHO
Isaya 41: 6-7
‘wakasaidiana, kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake; uwe na moyo mkuu.
   Seremala akamtia moyo mfua dhahabu na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga , akisema , ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike.
Ezra 10:4
Inuka maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu ukaitende.

MUNGU ATUSAIDIE TUSHIKAMANE TUYAKAMILISHE HAYA

IMETOLEWA NA UONGOZI USCF CHAS



No comments:

Post a Comment

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Yohana 3;16