KARIBU

KARIBU
Tunakusalimu katika Jina la BWANA wetu YESU KRISTO. karibu katika ukurasa huu maalumu wa USCF CCT UDOM CHAPLAINCY-KITIVO CHA TIBA. USCF ni kifupisho cha maneno machache; UNIVERSITY STUDENTS CHRISTIAN FELLOWSHIP na CCT ni kifupisho cha CHRISTIAN COUNCIL OF TANZANIA. Sisi ni ushirika wa vijana wa vyuo vikuu kutoka makanisa wanachama wa baraza la kikristo Tanzania (CCT). tumekuwa na ukurasa huu maalumu kwa ajili ya Kuhubiri Injili, Kufundisha Neno la Mungu, kupashana habari pamoja na kushauriana. Ni kiu yetu kuwa walioko makazini, majumbani, mashuleni na maeneo mbalimbali waweze kufikiwa na mahubiri/mafundisho yetu yanayotolewa na watumishi mbalimbali waliopo katikati yetu na wale wa nje ya USCF pamoja na wahubiri wa kimataifa. KARIBU TUJIFUNZE NA KUHABARIKA NA MUNGUAKUBARIKI

MAADHIMISHO YA KUUNDWA KWA CCT


 Mchungaji Kalinga katika ibada ya jumapili


Siku ya jumuiya ya kikisto Tanzania(CCT) Christrian council of Tanzania. Leo tar 22\0\2016, ni siku ya kuadhimisha siku ya kuundwa kwa jumuiya ya kikisto Tanzania.Christian council(CCT) iliyo anzishwa January 1963, na wa mishionary wa Lutheran, na Anglican.Mpaka sasa jumuiya ina makanisa washirika Lutheran church of Tanzania(ELCT), Anglican church Tanzania(ACT), Moravian church of Tanzania(MCT)< African Inland church Tanzania(AICT), Mennonote church in Tanzania(MCT), Baptist church in Tanzania(BCT), Salvation Army, African Brotherhood church, Church of God in Tanzania, Evangelistic church of Mbalizi. Mpaka leo tunafurahi kukaa kwenye umoja katika kristo yesu kama zaburi ya 133:1 inavyosema Tazama jinsi ilivo vemana kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja.

2 comments:

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Yohana 3;16