CHUO
KIKUU CHA DODOMA
UMOJA WA WANAFUNZI WA KIKRISTO
TANZANIA USCF-TIBA.
Bwana Yesu asifiwe,
Kama
tulivotangaziwa kuwa kuanzia tarehe 2 February hadi tarehe 5.february siku
ya jumapili tunatarajia kuwa na zoezi la
uchaguzi wa viongozi wapya ndani ya USCF-TIBA. Zoezi la uchaguzi litahusisha
chaguzi ndogo ndogo za vikundi mbalimbali ndani ya USCF ambazo zitafanyika
tarehe 2 siku ya alhamisi kwa upande wa PRAYS AND WORSHIP na kisha tarehe 4
siku ya jumamosi ni upande wa USCF KWAYA. Uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 5
jumapili, ambapo uchaguzi wa jumapili utahusisha ngazi zifuatazo:
KAMATI
KUU.
- Mwenyekiti
- Makamu mwenyekiti
- Katibu
- Katibu msaidizi
- Mtunza hazina.
KAMATI
YA MAOMBI.
- Mwenyekiti
- Katibu
KAMATI
YA UINJILISTI.
- Mwenyekiti
- Katibu
WAZEE
WA KANISA
- Kila block 1,2,.F,G,D,A na BCE.
SIFA ZA MTU ANAYESTAHILI
KUCHAGULIWA KATIKA NAFASI YA UONGOZI USCF.
- Awe mshiriki kamili wa makanisa yanayounda jumuiya ya umoja wa kikristo Tanzania (CCT). Kama vile
- Lutheran.
- Moravian.
- Anglican.
- Merronite.
- Baptist.
- Bible church Tanzania.
- Evangelist church of mbalizi. Na mengineyo.
- Asiwe finalist (Bsc.N4,Bsc.MW,DN3,PH3 MED LAB3) na pia asiwe MD3
- Asiwe mtu aliyewahi kukiuka taratibu,kanuni na maadili ya kikanisa kama vile.
- Kupata ujauzito nje ya ndoa
- Koa/kuolewa kinyume na taratibu za kanisa.
- Asiwe mtu aliyetengwa na kanisa kutokana na makosa ya kinidhamu.
- Awe na sifa za kushiriki meza ya bwana kutokana na taratibu za kanisa lake.
- Awe ni mtu ambaye una utayari wa kuwa kiongozi ndani ya USCF.
SIFA ZA MTU ANAYESTAHILI KUMCHAGUA
KIONGOZI KATIKA UCHAGUZI
- Awe mwana USCF
- Awe mtu ambaye anashirikiana na USCF katika vipindi vya ibada hata kama sio mwana USCF.
No comments:
Post a Comment