*MPENDWA NAKUKUMBUSHA TU* _*TUBU*_
👩msichana FACEBOOK Amepost picha amevaa nusu uchi badala umsaidie kujitambua Na namna ya
kujistili na kuvaa kwa heshima badala yake unamsifia! (Unasifia ujinga) unaanza,
*WOW Umependeza*
Mara *U are beautiful* Mara *I like it!* Ama *u look sexy!*
Wewe utakua sehem ya tatizo.
🗣 *_TUBU_* Mpendwa.
Hakua mke wako wa ndoa lakini ukafanya nae ngono, akapata mimba ukamwambia aitoe, Uzinzi/uasherati + Mauaji = Jehanam.
🗣 *_TUBU_* Mpendwa.
Tunasinzia wakati wa ibada lakini tunaweza kufuatilia tamthilia mpaka sa nane usiku, unachat Whatsapp hadi usiku wa manane na ni ngumu sana kupata japo dakika 30 za kuwasiliana na Mungu wako, utashangaa kuona MTU yuko active kwa social network
WhatsApp *last seen 1min ago*,
Facebook *last seen 2min ago*
Twitter *last seen 1min ago*
Instagram *Last seen 1min ago*
Bible/Biblia *Last seen 2014*
Wewe umekufa kiroho
🗣 _*TUBU*_ Mtu wa MUNGU.
Ni rahisi kufoward Ujumbe wa kuchekesha kwa marafiki zako kuliko Ujumbe wa neno la Mungu Kwanini?
🗣 *TUBU* Mpendwa.
Makanisani ni bure waumini ni wachache starehe ni malipo na kumbi zinajaa na wengine kukosa ticket ama sehem za kukaa
Uzima wa milele bure
Kuingia kanisa bure
Wokovu bure
Upendo wa Mungu bure
Pumzi ya uhai bure
Ni kwanini unaamua kulipia kwenda jehanam wakati peponi ni bure? 🗣 *TUBU* mtu wa MUNGU.
Mara nyingi tunakumbuka siku kama ya wapendanao, ya kuzaliwa, siku ya wanawake, siku ya watoto, boxing day, Christmas day, siku ya Uhuru, siku ya wakulima n.k lakini tunasahau siku ya HUKUMU itakuwaje? Itakua furaha au kulia na kusaga meno?
🗣 *TUBU* mpendwa.
Yeyote asie Mme/mke wako na anataka mfanye ngono kabla ya ndoa huyo ni Adui yako tena umkimbie kabisa, upendo wake ni feki sababu hakuna MTU anaekupenda kwa dhati anaetaka uende jehanam na kukosa pepo
🗣 *TUBU* kabisa mpenzi.
Unasema nataka nioe mke Mzuri/niolewe na handsome, ninunue gari zuri, ni jenge Nyumba nzuri Je hayo ndio unafikiria tu??? Hujui kama utakufa na utaviacha? Wekeza kwa Mungu.
🗣 *TUBU* mpendwa.
Makeup, mascara, wanja, lipstick, Powder, kope kubandika, mambo yote ya *Made in China* kama (kuongeza makalio n.k) yote ni bure kama MOYO wako hujaupamba kwa Tabia njema na hofu ya Mungu, bado utaonekana Mbaya tu! Jipambe kwa Tabia njema na kristo atawale na USO wako utang'ara automatically tu!
🗣 *TUBU* dada.
Je unadhani majuto ni pale ambapo hujaoa mke ulikua unamtaka? kuolewa na Mme uliemtaka? Ama nikutosoma course uloipenda? Hapana majuto ni pale utapoingia kaburini bila tumaini la kufufuliwa kwajili ya uzima wa milele.
🗣 *TUBU*
Hata uwe tajiri, masikin, mrembo, mwembamba, mnene, mfupi, mrefu, mbaya, mweusi, mweupe, ustazi, mchungaji, professor, mfalme, mtumwa, huru, n.k kifo hakijali wewe ni nani siku ikifika unakwenda. 🗣 acha kiburi, *TUBU*
Unaweza kuahirisha tarehe kama ya mahafali, ya harusi, ya uchaguzi, n.k lakini kamwe huwezi kuahirisha tarehe ya kufa kwako, siku zote kuwa tayari tengeneza na Mungu wako
🗣 *TUBU*
Wengine ni wagonjwa wewe ni mzima
Wengine wamekufa wewe unaishi
Wengine hawajala wewe umekula
Wengine wanahuzuni wewe una furaha
Wengine wamepata 1,000 wewe umepata elf 10,000 lakini mbona hauna shukrani kwa MUNGU?
🗣 *TUBU*
Ni ukarimu wa Mungu tu amekukirimia kwani wewe umefanya nini hata akukarimu? Mwambie Bwana Mimi si kitu si chochote ila nataka uzima wa Milele 🗣 *TUBU*
*KUMBUKA*:
_Toba ya kweli sio kulia machozi na baadae unaendelea na uovu wako Bali Toba ya kweli ni pale unapobadilika_
TUBU saivi, usingoje baadae.
*MUNGU KWANZA!!!*
No comments:
Post a Comment